Yohane 12:22-24
Yohane 12:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Filipo akaenda, akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu. Yesu akawaambia, “Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika! Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi.
Yohane 12:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
Yohane 12:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
Yohane 12:22-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu. Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.