Yeremia 51:63-64
Yeremia 51:63-64 Biblia Habari Njema (BHN)
Utakapomaliza kusoma kitabu hiki, kifungie jiwe, kisha ukitumbukize katikati ya mto Eufrate, ukisema: ‘Hivi ndivyo mji wa Babuloni utakavyozama, wala hautainuka tena, kwa sababu ya maafa ambayo Mwenyezi-Mungu anauletea.’” Mwisho wa maneno ya Yeremia.
Yeremia 51:63-64 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati; nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.
Yeremia 51:63-64 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati; nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.
Yeremia 51:63-64 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Utakapomaliza kusoma hiki kitabu, kifungie jiwe kisha ukitupe ndani ya Mto Frati. Kisha sema, ‘Hivi ndivyo Babeli utakavyozama na usiinuke tena, kwa sababu ya maafa nitakayoleta juu yake. Nao watu wake wataanguka.’ ” Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.