Yeremia 51:4-6
Yeremia 51:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo, watajeruhiwa katika barabara zake. Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli. Kimbieni kutoka Babuloni, kila mtu na ayaokoe maisha yake! Msiangamizwe katika adhabu yake, maana huu ndio wakati wa Mungu wa kulipa kisasi, anaiadhibu Babuloni kama inavyostahili.
Yeremia 51:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu. Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli. Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
Yeremia 51:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao wataanguka, hali ya kuuawa, katika nchi ya Wakaldayo, hali ya kutumbuliwa katika njia kuu zake. Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli. Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.
Yeremia 51:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wataanguka waliouawa katika Babeli, wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake. Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, BWANA Mwenye Nguvu Zote, ingawa nchi yao imejaa uovu mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. “Kimbieni kutoka Babeli! Okoeni maisha yenu! Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake. Ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa kile anachostahili.