Yeremia 51:36-37
Yeremia 51:36-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke. Babuloni itakuwa rundo la magofu, itakuwa makao ya mbweha, itakuwa kinyaa na kitu cha kuzomewa; hakuna mtu atakayekaa huko.
Yeremia 51:36-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu. Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.
Yeremia 51:36-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu. Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.
Yeremia 51:36-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa hiyo, hili ndilo BWANA asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake. Babeli utakuwa lundo la magofu na makao ya mbweha, kitu cha kutisha na kudharauliwa, mahali asipoishi mtu.