Yeremia 51:34-35
Yeremia 51:34-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme Nebukadneza wa Babuloni aliuharibu na kuuponda mji wa Yerusalemu aliuacha kama chungu kitupu; aliumeza kama joka. Alijaza tumbo lake vitu vyake vizurivizuri, akautupilia mbali kama matapishi. Watu wa Yerusalemu na waseme: “Babuloni na ulipizwe ukatili uleule, tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu! Babuloni ipatilizwe kwa umwagaji wa damu yetu.”
Yeremia 51:34-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniponda, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
Yeremia 51:34-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nebukadreza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniseta, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
Yeremia 51:34-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula, ametufanya tuchangayikiwe, ametufanya tuwe gudulia tupu. Kama nyoka ametumeza na kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri, kisha akatutapika. Jeuri iliyofanyiwa miili yetu na iwe juu ya Babeli,” ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni. “Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,” asema Yerusalemu.