Yeremia 51:31-33
Yeremia 51:31-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Tarishi baada ya tarishi wanapiga mbio, mjumbe mmoja anamfuata mjumbe mwingine, kumpasha habari mfalme wa Babuloni kwamba mji wake umevamiwa kila upande. Vivuko vya mto vimetekwa, ngome zimechomwa moto, askari wamekumbwa na hofu. Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: “Babuloni ni kama uwanja wa kupuria nafaka wakati unapotayarishwa. Lakini bado kidogo tu, wakati wa mavuno utaufikia.”
Yeremia 51:31-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tarishi mmoja atapiga mbio kumlaki mwingine, Na mjumbe mmoja atapiga mbio kumlaki mwenziwe, Ili kumpasha habari mfalme wa Babeli, Ya kuwa mji wake umetwaliwa kila upande. Navyo vivuko vimeshambuliwa, Nayo makangaga wameyatia moto, Nao watu wa vita wameingiwa na hofu. Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.
Yeremia 51:31-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tarishi mmoja atapiga mbio kumlaki mwingine, Na mjumbe mmoja atapiga mbio kumlaki mwenziwe, Ili kumpasha habari mfalme wa Babeli, Ya kuwa mji wake umetwaliwa kila upande. Navyo vivuko vimeshambuliwa, Nayo makangaga wameyatia moto, Nao watu wa vita wameingiwa na hofu. Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.
Yeremia 51:31-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tarishi mmoja humfuata mwingine, na mjumbe humfuata mjumbe, kumtangazia mfalme wa Babeli kwamba mji wake wote umetekwa, Vivuko vya mito vimekamatwa, mabwawa yenye mafunjo yametiwa moto, nao askari wameingiwa na hofu kuu.” Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria wakati inapokanyagwa; wakati wa kumvuna utakuja upesi.”