Yeremia 51:27-28
Yeremia 51:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Tweka bendera ya vita duniani, piga tarumbeta kati ya mataifa; yatayarishe mataifa kupigana naye; ziite falme kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Ashkenazi. Weka majemadari dhidi yake; walete farasi kama makundi ya nzige. Yatayarishe mataifa kupigana naye vita; watayarishe wafalme wa Medi, watawala na mawakili wao, tayarisheni nchi zote katika himaya yake.
Yeremia 51:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu. Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na watawala wake, na wakuu wake, na nchi yote ya mamlaka yake.
Yeremia 51:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu. Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na maliwali wake, na maakida wake, na nchi yote ya mamlaka yake.
Yeremia 51:27-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Twekeni bendera katika nchi! Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa! Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, iteni falme hizi dhidi yake: Ararati, Mini na Ashkenazi. Wekeni jemadari dhidi yake, pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige. Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, wafalme wa Wamedi, watawala wao na maafisa wao wote, pamoja na nchi zote wanazotawala.