Yeremia 51:20-23
Yeremia 51:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wewe Babuloni ni rungu na silaha yangu ya vita; nakutumia kuyavunjavunja mataifa, nakutumia kuangamiza falme. Nakutumia kuponda farasi na wapandafarasi, magari ya kukokotwa na waendeshaji wake. Ninakutumia kuwaponda wanaume na wanawake, wazee na vijana, wavulana na wasichana. Ninakutumia kuponda wachungaji na makundi yao, wakulima na wanyama wao wa kulimia, wakuu wa mikoa na madiwani.
Yeremia 51:20-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunjavunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunjavunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunjavunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe nitamvunjavunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunjavunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunjavunja watawala na makamanda.
Yeremia 51:20-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.
Yeremia 51:20-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wewe ndiwe rungu langu la vita, silaha yangu ya vita: kwa wewe navunjavunja mataifa, kwa wewe naangamiza falme, kwa wewe navunjavunja farasi na mpanda farasi, kwa wewe navunjavunja gari la vita na mwendeshaji wake, kwa wewe napondaponda mwanaume na mwanamke, kwa wewe napondaponda mzee na kijana, kwa wewe napondaponda kijana wa kiume na mwanamwali, kwa wewe nampondaponda mchungaji na kundi, kwa wewe nampondaponda mkulima na maksai, kwa wewe nawapondaponda watawala na maafisa.