Yeremia 51:17-18
Yeremia 51:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa, kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake; maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu, wala hazina pumzi ndani yake. Hazina thamani, ni udanganyifu mtupu; wakati watakapoadhibiwa, nazo zitaangamia.
Yeremia 51:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake. Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu; Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.
Yeremia 51:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)