Yeremia 51:13-14
Yeremia 51:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Nchi hiyo imejaa mito na hazina tele, lakini mwisho wake umefika, uzi wa uhai wake umekatwa. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake: “Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige, nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”
Yeremia 51:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ewe ukaaye juu ya maji mengi, uliye na hazina nyingi, mwisho wako umewadia, kadiri ya tamaa zako. BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.
Yeremia 51:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ewe ukaaye juu ya maji mengi, uliye na hazina nyingi, mwisho wako umewadia, kadiri ya tamaa zako. BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.
Yeremia 51:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wewe uishiye kando ya maji mengi na uliye na wingi wa hazina, mwisho wako umekuja, wakati wako wa kukatiliwa mbali. BWANA Mwenye Nguvu Zote ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: ‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige, nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’