Yeremia 51:11-12
Yeremia 51:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Noeni mishale yenu! Chukueni ngao! Twekeni bendera ya vita kushambulia kuta za Babuloni. Imarisheni ulinzi; wekeni walinzi; tayarisheni mashambulizi. Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekeleza mambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.
Yeremia 51:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake. Twekeni bendera ya vita juu ya kuta za Babeli, imarisheni ulinzi, wawekeni walinzi, tayarisheni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.
Yeremia 51:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake. Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli, yatieni malindo nguvu, wawekeni walinzi, tengenezeni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.
Yeremia 51:11-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Noeni mishale, chukueni ngao! BWANA amewaamsha wafalme wa Wamedi, kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. BWANA atalipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli! Imarisheni ulinzi, wekeni walinzi, andaeni waviziao! BWANA atatimiza kusudi lake, amri yake juu ya watu wa Babeli.