Yeremia 51:1-3
Yeremia 51:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni, dhidi ya wakazi wa Kaldayo. Nitawapeleka wapepetaji Babuloni, nao watampepeta; watamaliza kila kitu katika nchi yake watakapofika kuishambulia toka kila upande wakati wa maangamizi yake.” Usiwape nafasi wapiga mshale wa Babuloni; usiwaache wavute upinde, wala kuvaa mavazi yao ya vita. Usiwahurumie vijana wake; liangamize kabisa jeshi lake.
Yeremia 51:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli, na juu yao wakaao Leb-kamai, upepo uharibuo. Nami nitawatuma wapepetaji watakaompepea mpaka Babeli, nao wataifanya nchi yake kuwa tupu; kwa kuwa katika siku ya taabu watakuwa juu yake pande zote. Juu yake apindaye upinde, mwenye upinde na apinde upinde wake, na juu yake ajiinuaye katika dirii yake; msiwaachilie vijana wake; liangamizeni jeshi lake lote.
Yeremia 51:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli, na juu yao wakaao Leb-kamai, upepo uharibuo. Nami nitapeleka wageni mpaka Babeli, watakaompepea; nao wataifanya nchi yake kuwa tupu; kwa kuwa katika siku ya taabu watakuwa juu yake pande zote. Juu yake apindaye upinde, mwenye upinde na apinde upinde wake, na juu yake ajiinuaye katika dirii yake; msiwaachilie vijana wake; liangamizeni jeshi lake lote.
Yeremia 51:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi dhidi ya Babeli na watu wakaao Leb-Kamai. Nitawatuma wageni Babeli kumpepeta na kuiharibu nchi yake; watampinga kila upande katika siku ya maafa yake. Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake, wala usimwache avae silaha zake. Usiwaonee huruma vijana wake; angamiza jeshi lake kabisa.