Yeremia 5:27-28
Yeremia 5:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama vile kapu lililojaa ndege walionaswa, ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu. Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri, wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu maskini.
Yeremia 5:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Yeremia 5:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamewanda sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.