Yeremia 42:9-10
Yeremia 42:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli ambaye mlinituma kwake nipeleke maombi yenu, asema hivi: Kama mtabaki katika nchi hii, basi, nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawaotesha wala sitawangoa; kwa maana nitabadili nia kwa sababu ya maafa niliyowatenda.
Yeremia 42:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kwake, ili niyaweke maombi yenu mbele yake, asema hivi; Ikiwa mtabaki katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang'oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.
Yeremia 42:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kwake, ili niyaweke maombi yenu mbele yake, asema hivi; Ikiwa mtakaa bado katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang’oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.
Yeremia 42:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akawaambia, “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu: ‘Kama mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo.