Yeremia 42:3-4
Yeremia 42:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na atuoneshe njia anayotaka tuifuate, na kile anachotaka tukifanye.” Yeremia akawajibu, “Vema; nimesikia. Nitamwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kama mlivyonisihi; jibu lolote atakalonipa Mwenyezi-Mungu, nitawaambieni; sitawaficha chochote.”
Yeremia 42:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ili kwamba BWANA, Mungu wako, atuoneshe njia ambayo yatupasa tuiendee, na jambo litupasalo tulitende. Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lolote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote.
Yeremia 42:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ili kwamba BWANA, Mungu wako, atuonyeshe njia ambayo yatupasa tuiendee, na jambo litupasalo tulitende. Ndipo Yeremia, nabii, akawaambia, Nimewasikia; tazama, nitamwomba BWANA, Mungu wenu, sawasawa na maneno yenu; tena itakuwa, neno lo lote ambalo BWANA atawajibu, nitawaambia; sitawazuilia neno liwalo lote.