Yeremia 4:9-10
Yeremia 4:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.” Kisha nikasema: “Aa, Mwenyezi-Mungu, hakika umewadanganya kabisa watu hawa na mji wa Yerusalemu! Uliwaambia mambo yatawaendea vema, kumbe maisha yao yamo hatarini kabisa!”
Yeremia 4:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa. Nami nikasema, Aa, Bwana MUNGU! Hakika umewadanganya sana watu hawa na Yerusalemu, ukisema, Mtakuwa na amani lakini upanga umeingia katika nafsi za watu.
Yeremia 4:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa. Nami nikasema, Aa, Bwana MUNGU! Hakika umewadanganya sana watu hawa na Yerusalemu, ukisema, Mtakuwa na amani lakini upanga umeingia katika nafsi za watu.
Yeremia 4:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Katika siku ile,” asema BWANA “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.” Ndipo niliposema, “Aa, BWANA Mwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!”