Yeremia 4:5-6
Yeremia 4:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tangazeni huko Yuda, pazeni sauti huko Yerusalemu! Pigeni tarumbeta kila mahali nchini! Pazeni sauti na kusema: Kusanyikeni pamoja! Kimbilieni miji yenye ngome! Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni, kimbilieni usalama wenu, msisitesite! Mwenyezi-Mungu analeta maafa na maangamizi makubwa kutoka kaskazini.
Yeremia 4:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tangazeni katika Yuda, hubirini katika Yerusalemu, na kusema, Pigeni baragumu katika nchi, pigeni kelele sana, na kusema, Jikusanyeni pamoja, tukaingie katika miji yenye boma. Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamizi makuu.
Yeremia 4:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tangazeni katika Yuda, hubirini katika Yerusalemu, na kusema, Pigeni baragumu katika nchi, pigeni kelele sana, na kusema, Jikusanyeni pamoja, tukaingie katika miji yenye boma. Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamivu makuu.
Yeremia 4:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Tangaza katika Yuda na upige mbiu katika Yerusalemu na kusema: ‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’ Piga kelele na kusema: ‘Kusanyikeni pamoja! Tukimbilie katika miji yenye maboma!’ Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni! Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa! Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, maangamizi ya kutisha.”