Yeremia 4:31
Yeremia 4:31 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilisikia sauti kama ya mwanamke anayejifungua, yowe kama anayejifungua mtoto wa kwanza. Ilikuwa sauti ya Yerusalemu akitweta, na kuinyosha mikono yake akisema, ‘Ole wangu! Wanakuja kuniua!’”
Yeremia 4:31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.
Yeremia 4:31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa utungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.
Yeremia 4:31 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nasikia kilio kama cha mwanamke katika utungu wa kuzaa, kilio cha uchungu kama cha anayemzaa mtoto wake wa kwanza: kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua, akiinua mikono yake, akisema, “Ole wangu! Ninazimia; maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”