Yeremia 4:3-4
Yeremia 4:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu: “Limeni mashamba yenu mapya; msipande mbegu zenu penye miiba. Enyi watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, jitakaseni kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu, wekeni mioyo yenu wazi mbele yangu. La sivyo, ghadhabu yangu itachomoza kama moto, iwake hata pasiwe na mtu wa kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Yeremia 4:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba. Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Yeremia 4:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba. Jitahirini kwa BWANA, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Yeremia 4:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo asemalo BWANA kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu: “Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu, wala msipande katikati ya miiba. Jitahirini katika BWANA, tahirini mioyo yenu, enyi wanaume wa Yuda na watu wa Yerusalemu, la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvu na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mliotenda, ikiwaka pasipo wa kuizima.