Yeremia 32:26-28
Yeremia 32:26-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Tazama, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa watu wote. Hakuna lolote linaloweza kunishinda. Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ninautoa mji huu kwa Wakaldayo na kwa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, naye atauteka.
Yeremia 32:26-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza? Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitautia mji huu katika mikono ya Wakaldayo, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, naye atautwaa
Yeremia 32:26-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitautia mji huu katika mikono ya Wakaldayo, na katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, naye atautwaa
Yeremia 32:26-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: “Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza? Kwa hiyo, hili ndilo asemalo BWANA: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa Wakaldayo, na mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ambaye atauteka.