Yeremia 2:9-10
Yeremia 2:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema, “Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi, na nitawalaumu wazawa wenu. Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone, au tumeni watu huko Kedari wakachunguze, kama jambo kama hili limewahi kutokea
Yeremia 2:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu. Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wowote.
Yeremia 2:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu. Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wo wote.
Yeremia 2:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema BWANA. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.