Yeremia 2:34-35
Yeremia 2:34-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Nguo zako zina damu ya maskini wasio na hatia, japo hukuwakuta wakivunja nyumba yako. “Lakini licha ya hayo yote, wewe wasema: ‘Mimi sina hatia; hakika hasira yake imegeuka mbali nami.’ Lakini mimi nitakuhukumu kwa sababu unasema: ‘Sikutenda dhambi.’
Yeremia 2:34-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena katika pindo za nguo zako imeonekana damu ya roho zao maskini wasio na hatia; sikuiona penye mahali palipobomoka, lakini niliiona juu ya hawa wote. Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.
Yeremia 2:34-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena katika pindo za nguo zako imeonekana damu ya roho zao maskini wasio na hatia; sikuiona penye mahali palipobomoka, lakini naliiona juu ya hawa wote. Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.
Yeremia 2:34-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Katika nguo zako watu huona damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. Lakini katika haya yote unasema, ‘Sina hatia; Mungu hajanikasirikia.’ Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, ‘Mimi sijatenda dhambi.’