Yeremia 2:32-33
Yeremia 2:32-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Kijana msichana aweza kusahau mapambo yake au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau kwa muda wa siku zisizohesabika. Kweli wewe ni bingwa wa kutafuta wapenzi! Hata wanawake wabaya huwafundisha njia zako.
Yeremia 2:32-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu. Jinsi ulivyoitengeneza njia yako ili kutafuta mapenzi! Kwa sababu hiyo hata wanawake wabaya umewafundisha njia zako.
Yeremia 2:32-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu. Jinsi ulivyoitengeneza njia yako ili kutafuta mapenzi! Kwa sababu hiyo hata wanawake wabaya umewafundisha njia zako.
Yeremia 2:32-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Je, mwanamwali husahau vito vyake, au bibi arusi mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu. Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! Hata wale wanawake wabaya kuliko wote wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.