Yeremia 2:22-23
Yeremia 2:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata ukijiosha kwa magadi, na kutumia sabuni nyingi, madoa ya uovu wako bado yatabaki mbele yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Unawezaje kusema, ‘Mimi si najisi; sijawafuata Mabaali?’ Tazama ulivyotenda dhambi kule bondeni; angalia ulivyofanya huko! Wewe ni kama mtamba wa ngamia, akimbiaye huko na huko
Yeremia 2:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema Bwana MUNGU. Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake
Yeremia 2:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema Bwana MUNGU. Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake
Yeremia 2:22-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hata ujisafishe kwa magadi na kutumia sabuni nyingi, bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” asema BWANA Mwenyezi. “Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi, sijawafuata Mabaali’? Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni; fikiri uliyoyafanya. Wewe ni ngamia jike mwenye mbio ukikimbia hapa na pale