Yeremia 2:16-18
Yeremia 2:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi, wameuvunja utosi wake. Israeli, je, hayo yote si umejiletea mwenyewe, kwa kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekuwa ninakuongoza njiani? Na sasa itakufaa nini kwenda Misri, kunywa maji ya mto Nili? Au itakufaa nini kwenda Ashuru, kunywa maji ya mto Eufrate?
Yeremia 2:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena wana wa Nofu na Tapanesi wamevunja utosi wa kichwa chako. Je! Hukujipatia mambo haya mwenyewe, kwa kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, alipokuongoza njiani? Na sasa una nini utakayofaidi katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayofaidi katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?
Yeremia 2:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena wana wa Nofu na Tahpanesi wamevunja utosi wa kichwa chako. Je! Hukujipatia mambo haya mwenyewe, kwa kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, alipokuongoza njiani? Na sasa una nini utakayotenda katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayotenda katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?
Yeremia 2:16-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesi wamevunja taji ya kichwa chako. Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe kwa kumwacha BWANA, Mungu wako alipowaongoza njiani? Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori? Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto Frati?