Yeremia 2:12-13
Yeremia 2:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Shangaeni enyi mbingu, juu ya jambo hili, mkastaajabu na kufadhaika kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana, watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.
Yeremia 2:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuwa ukiwa sana, asema BWANA. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.
Yeremia 2:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuwa ukiwa sana, asema BWANA. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
Yeremia 2:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema BWANA. “Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.