Yeremia 2:1-2
Yeremia 2:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia: “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana, jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako, ulivyonifuata jangwani kwenye nchi ambayo haikupandwa kitu.
Yeremia 2:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.
Yeremia 2:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likanijia, kusema, Enenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa uposo wako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.
Yeremia 2:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Neno la BWANA lilinijia kusema, “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.