Isaya 66:7-8
Isaya 66:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mji wangu mtakatifu, ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu; kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto. Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.
Isaya 66:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kabla hajawa na uchungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto wa kiume. Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipopata uchungu, Alizaa watoto wake.
Isaya 66:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume. Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.
Isaya 66:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kabla hajasikia utungu, alizaa; kabla hajapata maumivu, alizaa mtoto mwanaume. Ni nani amepata kusikia jambo kama hili? Ni nani amepata kuona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja, au taifa laweza kutokea mara? Mara Sayuni alipoona utungu, alizaa watoto wake.