Isaya 66:3-4
Isaya 66:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: Wananitolea tambiko ya ng'ombe na mara wanaua watu kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwanakondoo na pia wanamvunja mbwa shingo. Wananitolea tambiko ya nafaka na pia kupeleka damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe. Basi, nitawaletea taabu; yatawapata yaleyale wanayoyahofia; maana nilipoita hakuna aliyeitika, niliponena hawakusikiliza. Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu, walichagua yale ambayo hayanipendezi.”
Isaya 66:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao. Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.
Isaya 66:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao. Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.
Isaya 66:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali, nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa. Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu, niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza. Walifanya maovu machoni pangu na kuchagua lile linalonichukiza.”