Isaya 66:15-16
Isaya 66:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto. Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
Isaya 66:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Isaya 66:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Isaya 66:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tazama, BWANA anakuja na moto, magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli, atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali, na karipio lake pamoja na miali ya moto. Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake BWANA atatekeleza hukumu juu ya watu wote, nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na BWANA.