Isaya 40:23-24
Isaya 40:23-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu. Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota, hata kabla hawajatoa mizizi kama miti udongoni, Mwenyezi-Mungu akiwapulizia hunyauka, kimbunga huwapeperusha kama makapi!
Isaya 40:23-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
Isaya 40:23-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
Isaya 40:23-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Huwafanya wakuu kuwa si kitu, na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure. Mara baada ya kupandwa, mara baada ya kutiwa ardhini, mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini, ndipo huwapulizia nao wakanyauka, nao upepo wa kisulisuli huwapeperusha kama makapi.