Isaya 40:15-16
Isaya 40:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, ni kama vumbi juu ya mizani. Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini. Kuni zote za Lebanoni na wanyama wake wote havitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.
Isaya 40:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana. Lebanoni nao hautoshelezi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara.
Isaya 40:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana. Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara.