Isaya 30:8-11
Isaya 30:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu aliniambia: “Sasa chukua kibao cha kuandikia, uandike jambo hili mbele yao, liwe ushahidi wa milele: Watu hawa ni waasi, watoto wasioaminika; watu wasiopenda kusikia mafunzo ya Mwenyezi-Mungu. Huwaambia waonaji: ‘Msione maono’, na manabii: ‘Msitutangazie ukweli, bali tuambieni mambo ya kupendeza, toeni unabii wa mambo ya udanganyifu tu. Geukeni na kuiacha njia ya ukweli; msituambie tena juu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.’”
Isaya 30:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya, nenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele. Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA; wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo; tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.
Isaya 30:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya, enenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele. Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA; wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo; tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.
Isaya 30:8-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao, liandike kwenye kitabu, ili liweze kuwa shahidi milele kwa ajili ya siku zijazo. Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya BWANA. Wanawaambia waonaji, “Msione maono tena!” Nako kwa manabii wanasema, “Msiendelee kutupatia maono ambayo ni ya kweli! Tuambieni mambo ya kupendeza, tabirini mambo ya uongo. Acheni njia hii, ondokeni katika mapito haya, nanyi acheni kutukabili pamoja na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”