Isaya 30:3-5
Isaya 30:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu, na usalama nchini Misri utakuwa fedheha yenu. Maana ingawa maofisa wao wamefika Soani, na wajumbe wao mpaka Hanesi, wote wataaibishwa na hao wasioweza kuwasaidia, watu ambao hawawezi kuwapa msaada au faida, ila tu kuwapa aibu na fedheha.”
Isaya 30:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, nguvu za Farao zitakuwa aibu yenu, na kutumainia kivuli cha Misri kutakuwa aibu yenu. Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi. Wote watawaonea haya watu wasioweza kuwafaidia, wasio na msaada wala faida, bali ni aibu na sababu ya kushutumiwa.
Isaya 30:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, nguvu za Farao zitakuwa aibu yenu, na kutumainia kivuli cha Misri kutakuwa kufadhaika kwenu. Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi. Wote watawaonea haya watu wasioweza kuwafaidia, wasio na msaada wala faida, bali ni aibu na sababu ya kushutumiwa.
Isaya 30:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu, kivuli cha Misri kitawaletea fedheha. Ingawa wana maafisa katika Soani na wajumbe wamewasili katika Hanesi, kila mmoja ataaibishwa kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu, ambalo haliwaletei msaada wala faida, bali aibu tu na fedheha.”