Isaya 30:27-28
Isaya 30:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Tazameni, Mwenyezi-Mungu mwenyewe anakuja toka mbali! Amewaka hasira na moshi wafuka; midomo yake yaonesha ghadhabu yake, maneno anayosema ni kama moto uteketezao. Pumzi yake ni kama mafuriko ya mto ambao maji yake yanafika hadi shingoni. Anakuja kuyachekecha mataifa kwa chekecheke ya maangamizi, kuwafunga lijamu na kuwapeleka wasikotaka.
Isaya 30:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, jina la BWANA linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto uangamizao; na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.
Isaya 30:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, jina la BWANA linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto ulao; na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.
Isaya 30:27-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tazama, Jina la BWANA linakuja kutoka mbali, likiwa na hasira kali inayowaka pamoja na wingu zito la moshi, midomo yake imejaa ghadhabu na ulimi wake ni moto ulao. Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi, yakipanda hadi shingoni. Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu, huweka lijamu katika mataya ya mataifa ambayo huwaongoza upotevuni.