Isaya 11:4-5
Isaya 11:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Atawapatia haki watu maskini, atawaamulia sawasawa wanyonge nchini. Kwa neno lake ataiadhibu dunia, kwa tamko lake atawaua waovu. Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga, uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
Isaya 11:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.
Isaya 11:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)