Ezekieli 10:20-22
Ezekieli 10:20-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Hawa walikuwa wale viumbe hai niliowaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na mto Kebari, nami nikatambua kuwa ni viumbe wenye mabawa. Kila mmoja wao alikuwa na nyuso nne na mabawa manne; na chini ya kila bawa kulikuwa na kitu kama mkono wa binadamu. Vilevile nilizitambua nyuso zao: Zilikuwa zilezile nilizokuwa nimeziona kule kwenye mto Kebari. Kila kiumbe alikwenda mbele, moja kwa moja.
Ezekieli 10:20-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Huyu ndiye kiumbe hai niliyemwona, chini ya Mungu wa Israeli, karibu na mto Kebari; nikajua ya kuwa hao ni makerubi. Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne; na mifano ya mikono ya mwanadamu ilikuwa chini ya mabawa yao. Na mfano wa nyuso zao, ni nyuso zile zile nilizoziona karibu na mto Kebari; kuonekana kwao, na wao wenyewe; kila mmoja walikwenda mbele moja kwa moja.
Ezekieli 10:20-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Huyu ndiye kiumbe hai niliyemwona, chini ya Mungu wa Israeli, karibu na mto Kebari; nikajua ya kuwa hao ni makerubi. Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne; na mifano ya mikono ya mwanadamu ilikuwa chini ya mabawa yao. Na mfano wa nyuso zao, ni nyuso zile zile nilizoziona karibu na mto Kebari; kuonekana kwao, na wao wenyewe; kila mmoja walikwenda mbele moja kwa moja.
Ezekieli 10:20-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hawa walikuwa ndio viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua ya kuwa hao walikuwa makerubi. Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, mabawa manne, chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu. Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alikwenda mbele moja kwa moja.