Kutoka 7:22-25
Kutoka 7:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wachawi wa Misri kwa kutumia uchawi wao wakafanya vivyo hivyo. Kwa hiyo moyo wa Farao ukabaki kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni; ikawa kama Mwenyezi-Mungu alivyokuwa amesema. Basi, Farao akarudi nyumbani kwake, na hata haya yaliyotokea hakuyajali. Wamisri wote wakachimbachimba kandokando ya mto Nili ili wapate maji ya kunywa, kwani hawakuweza kunywa maji ya mto huo. Pigo hilo la mto Nili lilidumu siku saba.
Kutoka 7:22-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena. Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni. Wamisri wote wakachimbachimba kando ya mto ili wapate maji ya kunywa; maana, hawakuweza kuyanywa yale maji ya mtoni. Zikatimia siku saba, baada ya BWANA kuupiga ule mto.
Kutoka 7:22-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena. Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni. Wamisri wote wakachimba-chimba kando ya mto ili wapate maji ya kunywa; maana, hawakuweza kuyanywa yale maji ya mtoni. Zikatimia siku saba, baada ya BWANA kuupiga ule mto.
Kutoka 7:22-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile BWANA alivyokuwa amesema. Badala yake, Farao akageuka, akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni. Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Naili kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto. Zilipita siku saba baada ya BWANA kuyapiga maji ya Mto Naili.