Kumbukumbu la Sheria 4:3-4
Kumbukumbu la Sheria 4:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyinyi mliona kwa macho yenu mambo ambayo Mwenyezi-Mungu aliyafanya kuhusu Baal-peori. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliwaangamiza watu wote miongoni mwenu waliomwabudu huyo mungu Baal-peori. Lakini nyinyi mliokuwa waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mko hai hadi leo.
Kumbukumbu la Sheria 4:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako. Bali ninyi mlioambatana na BWANA, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo.
Kumbukumbu la Sheria 4:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako. Bali ninyi mlioambatana na BWANA, Mungu wenu, mnaishi kila mmoja wenu, hata leo.
Kumbukumbu la Sheria 4:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mliona kwa macho yenu wenyewe kile BWANA alichokifanya kule Baal-Peori. BWANA Mungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori, lakini ninyi nyote mlioshikamana na BWANA kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.