Kumbukumbu la Sheria 4:16-18
Kumbukumbu la Sheria 4:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
msipotoke kwa kujifanyia sanamu yoyote ya kuchonga, au ya umbo au mfano wowote, mfano wa kiume au wa kike, wa mnyama yeyote duniani au ndege, au mfano wa mnyama atambaaye ardhini au wa samaki majini.
Kumbukumbu la Sheria 4:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yoyote, mfano wa mwanamume au mwanamke, mfano wa mnyama yeyote aliye duniani, au mfano wa ndege yeyote arukaye mbinguni, au mfano wa kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki yeyote aliye katika maji chini ya nchi
Kumbukumbu la Sheria 4:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke, mfano wa mnyama ye yote aliye duniani, au mfano wa ndege ye yote arukaye mbinguni, au mfano wa kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki ye yote aliye majini chini ya nchi
Kumbukumbu la Sheria 4:16-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke, au kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege yeyote arukaye angani, au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji.