Kumbukumbu la Sheria 4:13-14
Kumbukumbu la Sheria 4:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Naye akawatangazia agano lake akawaamuru mlishike yaani mzitii zile amri kumi ambazo aliziandika juu ya vibao viwili vya mawe. Wakati huo Mwenyezi-Mungu aliniamuru niwafundishe masharti na maagizo yote ambayo mnapaswa kuyatekeleza katika nchi mnayokwenda kuimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 4:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawahubiria agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika katika vibao viwili vya mawe. BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 4:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe. BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Aliwatangazia Agano lake na Amri Kumi, ambazo aliwaamuru mzifuate, kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe. Naye BWANA alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.