Kumbukumbu la Sheria 30:11-14
Kumbukumbu la Sheria 30:11-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.
Kumbukumbu la Sheria 30:11-14 Biblia Habari Njema (BHN)
“Amri ninazowapa leo si ngumu mno kwenu, wala haziko mbali nanyi. Haziko mbinguni hata mseme, ‘Nani atakayepanda juu mbinguni kutuletea ili tupate kuzisikia na kuzitii?’ Wala haziko ngambo ya bahari, hata mseme, ‘Nani atakayevuka bahari atuletee ili tuzisikie na kuzitii.’ Sivyo, ila zipo karibu nanyi, vinywani mwenu na mioyoni mwenu, mpate kuzitekeleza.
Kumbukumbu la Sheria 30:11-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? Wala si ng'ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.
Kumbukumbu la Sheria 30:11-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.