Kumbukumbu la Sheria 28:9-10
Kumbukumbu la Sheria 28:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mwenyezi-Mungu atawafanyeni kuwa watu wake watakatifu kama alivyowaahidi, kama mkizitii amri zake yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake. Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.
Kumbukumbu la Sheria 28:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.
Kumbukumbu la Sheria 28:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.
Kumbukumbu la Sheria 28:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya BWANA Mungu wako na kwenda katika njia zake. Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la BWANA, nao watakuogopa.