Kumbukumbu la Sheria 13:12-13
Kumbukumbu la Sheria 13:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mtakapoishi katika miji ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapa, huenda mkasikia kuwa watu fulani mabaradhuli miongoni mwenu, wamewashawishi watu wa mji wakisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine,’ miungu ambayo bado hamjawahi kuijua
Kumbukumbu la Sheria 13:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo BWANA, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa, Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua
Kumbukumbu la Sheria 13:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo BWANA, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa, Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua
Kumbukumbu la Sheria 13:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayo BWANA Mungu wenu anawapa mkae ndani yake kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu)