Danieli 6:4
Danieli 6:4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wale wakuu pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumshtaki Danieli kuhusu mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumlaumu, wala kosa lolote, kwani Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala hatia yoyote.
Danieli 6:4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi mawaziri na viongozi wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Danieli 6:4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Danieli 6:4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Walipofahamu hilo, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe.