Matendo 20:13-14
Matendo 20:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi kavu. Basi, alitukuta kule Aso, tukampandisha melini, tukaenda Mitulene.
Matendo 20:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimia kwenda kwa miguu. Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.
Matendo 20:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu. Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.