Matendo 19:37-39
Matendo 19:37-39 Biblia Habari Njema (BHN)
Mmewaita watu hawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumba ya mungu wala kumtukana mungu wetu wa kike. Kama, basi Demetrio na wafanyakazi wake wana mashtaka yao kuhusu watu hawa, yapo mahakama na wakuu wa mikoa; wanaweza kushtakiana huko. Kama mna matatizo mengine, yapelekeni katika kikao halali.
Matendo 19:37-39 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasioiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu. Basi ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja naye wana neno juu ya mtu yeyote, baraza ziko, na watawala wako; na washitakiane. Ikiwa kuna mambo mengine yoyote mnayotaka kujua, ni sharti yasuluhishwe katika kusanyiko lililo halali.
Matendo 19:37-39 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana mmewaleta watu hawa, wasioiba vitu vya hekalu wala kumtukana mungu mke wetu. Basi ikiwa Demetrio na mafundi walio pamoja naye wana neno juu ya mtu, baraza ziko, na maliwali wako; na washitakiane. Bali mkitafuta neno lo lote katika mambo mengine, yatatengenezwa katika kusanyiko lililo halali.
Matendo 19:37-39 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa kuwa mmewaleta hawa watu hapa, ingawa hawajaiba hekaluni wala kumkufuru huyu mungu wetu wa kike. Basi, ikiwa Demetrio na mafundi wenzake wana jambo zito dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na wasaidizi wa mwakilishi wa mtawala. Wanaweza kufungua mashtaka. Lakini kama kuna jambo jingine lolote zaidi mnalotaka kulileta, itabidi lisuluhishwe katika kusanyiko halali.