Matendo 19:30-32
Matendo 19:30-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia. Maofisa wengine wa huo mkoa wa Asia, waliokuwa rafiki zake, walimpelekea Paulo ujumbe wakimsihi asijihatarishe kwa kwenda kwenye ukumbi wa michezo. Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
Matendo 19:30-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na Paulo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. Na baadhi ya wakuu wa Asia, walio rafiki zake, wakatuma watu kwake, wakimsihi asiingie ndani katika ukumbi wa michezo. Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafukachafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.
Matendo 19:30-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na Paulo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie. Na baadhi ya wakuu wa Asia, walio rafiki zake, wakatuma watu kwake, wakimsihi asijihudhurishe nafsi yake ndani ya mahali pa michezo. Basi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi; kwa maana ule mkutano ulikuwa umechafuka-chafuka, na wengi wao hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.
Matendo 19:30-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Paulo akataka kuingia katikati ya umati huo, lakini wanafunzi hawakumruhusu. Hata baadhi ya viongozi wa sehemu ile, waliokuwa rafiki zake Paulo, wakatuma watu wakitamani asiingie katika ule ukumbi. Ule umati ulikuwa na taharuki. Wengine walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko.