2 Timotheo 1:3-4
2 Timotheo 1:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka katika sala zangu usiku na mchana. Nakumbuka machozi yako na ninatamani sana kukuona, ili nijazwe furaha.
2 Timotheo 1:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. Nikiyakumbuka machozi yako, natamani sana kukuona, ili nijawe na furaha
2 Timotheo 1:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha