2 Timotheo 1:15-18
2 Timotheo 1:15-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama unavyojua, watu wote mkoani Asia wameniacha, miongoni mwao wakiwa Fugelo na Hermogene. Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni, ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafuta kwa bidii mpaka akanipata. Bwana amjalie kupata huruma ya Mungu katika siku ile! Nawe wajua vizuri mengi aliyonifanyia huko Efeso.
2 Timotheo 1:15-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene. Bwana awape rehema wale walio wa jamaa wa Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu; bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii na kunipata. Bwana na amjalie ili kwamba apate rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana.
2 Timotheo 1:15-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene. Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu; bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata. Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana.
2 Timotheo 1:15-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene. Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.